Jumatatu , 10th Apr , 2023

Takriban watu watano wamefariki dunia na mtu mmoja hajulikani alipo baada ya kuanguka kwa barafu  katika milima ya Alps ya Ufaransa.Tukio hilo lilitokea  kusini mashariki mwa Ufaransa majira ya mchana jumapili saa za eneo hilo.

Naibu meya, Élisabeth Mollard, amethibitisha vifo hivyo na kukiambia kituo cha redio cha Ufaransa kwamba  wawili kati ya waliofariki ni viongozi wa eneo hilo.Watu wengine kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini.

Aajali  hiyo imesababishwa na theluji iliyojitenga kutoka juu ya mlima,  Vikosi vya uokoaji milimani vimeungana na mbwa wa utafutaji na uokoaji walipokuwa wakifanya kazi siku nzima kujaribu kuwafikia wale waliokwama. Juhudi za kumtafuta mtu aliyepotea zinatarajiwa kuanza tena Jumatatu.

 Mmoja wa mashuhuda aliiambia Televisheni ya Ufaransa kwamba alikuwa akitembea kwa miguu mbele tu ya glacier ya Armancette alipoona anguko la barafu likitokea na kuchukua simu yake kuipiga picha.

Wanaoserereka kwenye barafu katika  za skii zilizoandaliwa wametakiwa kuwa waangalifu.