Wananchi wakiomboleza msibani kwa Akwii alie uwawa kwa kupigwa kwa kitu kinachosadikika kuwa ni nondo kichwani
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba Akwii alikwenda kusuluhisha ugomvi uliokuwa wa mda mrefu kati ya wapenzi hao kitendo ambacho kijana mwenye mchumba hakufurahishwa na kitendo hicho na baadae kurudi na kuamua kumpiga na nondo na hatimae kupelekea umauti wake.
“Huyu ni mzee mlinzi wa kijiji hapa ameuwawa aliingilia ugomvi wa mdada ambae alikuwa akigombana na mme wake. Yeye alikwenda kumfata mlinzi mwenzake usiku na wakati wanarudi lindoni kwake wakakuta ugomvi usiku ndo akamwambia mwanaume acha kugombana na huyo dada huku akimtetea na ndipo mwanaume akamuweka alama akaja baadae akamvizia na kumpiga na nondo akafariki” Amesema David mkazi wa Kimandolu
Wakazi wa kimandolu wameeleza kuguswa na kifo cha mlinzi huyo na tayari tukio hilo limesharipotiwa kituo cha polisi kwa ajili ya uchunguzi Zaidi.