Moja ya Athari za El Nino kwa nchi za Kiafrika.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya tathimini ya athari za El Niño kwa Afrika iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.
Shirika hilo linasema Kusini mwa Afrika inakadiriwa kwamba watu milioni 21.7 watahitaji msaada wa chakula, na wadau wa misaada wanapanga kuwasaidia watu milioni 12.8 katika mataifa yaliyoathirika zaidi ya Angola, Lesotho, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Swaziland na Zimbabwe.
Mataifa mengine yanayohitaji msaada ni Ethiopia, Sudan na Somalia.