Jumanne , 22nd Nov , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha kamishna Diwan Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 22,2016

Hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Diwani Athuman Msuya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene,  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu na Makamishna wa Polisi.

Baada ya kuapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili, Idara ya Viongozi wa Siasa Bw. Waziri Yahaya Kipacha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali mara baada ya kumwapisha kamishna Diwan Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 22,2016

Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Amantius Msole ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiteta jambo na kuagana na kamishna Diwan Athumani mara baada ya kumwapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 22,2016