Ijumaa , 4th Jul , 2025

Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la kiwango cha umaskini nchini, akiongea na wananchi wa Tabora amesema kuwa hali imezidi kuwa mbaya licha ya rasilimali lukuki zilizopo kwenye baadhi ya mikoa.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mkoa wa Tabora, Zitto amesema kuwa idadi ya Watanzania wanaoishi katika dimbwi la umaskini imeongezeka kutoka watu milioni 14 mwaka 2020 hadi kufikia watu milioni 26 mwaka 2025.

Kwa mujibu wa takwimu alizozitoa, asilimia 33 ya wakazi wa Tabora wanaishi chini ya mstari wa umaskini, jambo alilolitaja kuwa ni aibu kwa taifa lenye utajiri wa rasilimali asilia.