Ijumaa , 24th Mar , 2023

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjato Kasilda Mgeni ameagiza Askari wa Wanyama pori kuhamishia kituo cha kuzuia Wanyama kijiji cha Muhesa Kata ya Maore ili kurahisha kazi ya kudhibiti tembo ambao wanatoka katoka hifadhi ya Taifa Mkomazi na kuingia katika kijiji hicho 

Pia mkuu huyo wa Wilaya amewataka Askari kufanya kazi kwa uadilifu kuwa na ukaribu na viongozi wa Vijiji ambavyo vinazunguuka hifadhi hiyo Ili waweze kupata taarifa kwa urahisi, wakati mipango mingine ikiendelea ikiwemo kupata Vilipuzi kusaidia kuzuia Tembo wasiingie kwenye vijiji hivyo na kuharibu mazao ya wakulima.

Maagizo hayo yamekuja kufuatia malalamiko ya wakazi wa kijiji hicho, kudai Maisha yao yapo hatarini kitokana na kuwepo kwa makundi makubwa ya Tembo wanaoingia kwenye maeneo ambayo kunafanyika shughuli za kibinadamu IKIWEMO Kilimo, huku tembo hao wakiwajeruhi baadhi ya watu, Kuuawa na wengine kuharibiwa Mazao yao.

"Sisi sio wakutegemea vyakula vya msaada, Mhe.Mkuu wa Wilaya tunatambua umuhimu wa Wanyama na maeneo ya hifadhi lakini kinacho endelea sasa tunaomba Serikali ifanye kila kinacho wezekana mtusaidie Tembo wasituharibie Mazao yetu Hali ni mbaya na hatujui itakuaje kama Wanyama hawa hawatudhinitiwa". Alisema mmoja wakazi wa kijiji hicho.