
Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,imesema kuwa asilimia 48 ya wanawake bado wanajifungulia majumbani na kuwa ni mojawapo ya sababu ya kuongezeka kwa vifo vya mama na watoto pamoja na kuongezeka kwa ugonjwa wa fistula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesema hayo wakati wa maswali na majibu Bungeni Mjini Dodoma na kusema kuwa wizara hiyo itaendelea kutoa elimu yakutosha kwa wajawazito kujifungulia hospitalini ili kusaidia katika jitihada za kupunguza ugonjwa wa fistula unaowatesa wanawake wengi nchini.
Mh Ummy ameongeza kuwa jitihada kubwa serikali inazofanya ni pamoja na kutoa motisha kwa wanawake wajawazito ikiwemo kutoa huduma ya bure ya vifaa vya kujifungulia kwa wanawake 500 na kuboresha huduma za upasuaji wa fistula.
Aidha amesema kuwampango wa wizara yake ni kutoa elimu yakutosha kwa wakunga wa jadi ili waweze kuwaongoza wanawake hao kwaajili ya kwenda kujifungulia hospitalini.