Kwa mujibu wa wakili wake Lucie Simon, amesema mwanaume huyo bado yuko hospitalini na korodani zake zililazimika kukatwa kutokana na kipigo kikali na kwamba atawasilisha malalamishi kwa niaba ya mteja wake ambaye ni mhandisi mwenye umri wa miaka 26.
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema kuwa takriban Wafaransa 80,000 waliandamana mjini Paris wiki iliyopita kama sehemu ya maandamano ya nchi nzima kupinga mpango wa Rais Emmanuel Macron wa kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64