
Tukio hilo limetokea leo mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT), ambao umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika mkutano huo mama Anna Mghwira amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona jitihada za CCM katika kuleta maendeleo, hivyo akaona ni vyema akajiunga nao.
"Mimi baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kwa muda mfupi nimeona mengi ndani ya CCM na nimeona sio mbaya nikitamka kuwa naungana nanyi rasmi, wa muda mfupi nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa letu mbeleahsanteni sana kwa kunipokea na kama niliposikia hotuba ya Mwenyekiti ni kweli kuwa sisi akina mama ndiyo wenye jukumu la kubeba nchi. Na mimi naungana na akina mama wenzangu wa UWT wenye malengo ya kuendeleza taifa", amesema mama Anna Mghwira.
Mama Anna Mghwira anakuwa kiongozi mkubwa wa tatu kitaifa wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM ndani ya mwaka huu.