Jumapili , 4th Mei , 2025

Kaka wa Kajala Bilionea Saidi Lugumi amesisitiza ndoa kati ya Marioo na Paulah kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wao Amarah ambaye ametimiza mwaka mmoja.

Picha ya Saidi Lugumi akizunguma na Marioo na Paulah kuhusu ndoa

Lugumi amemtaka Marioo kutekeleza wale waliyokubaliana kama familia sababu hata mwanzo alikuwa anataka waoane kwanza kisha waingie kwenye uzazi.

Mastaa waliohudhuria katika sherehe ya mtoto wa #Marioo na #Paulah kutimiza mwaka mmoja ni Harmonize,Billnass, Nandy,P Funk Majani, Kajala (Babu na Bibi Amarah) DogoPaten, Hamisa Mobetto, Wolper, Zaylissa, Lulu Diva, Angle Nyigu na Team Lamata.