Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Katika hali isiyokuwa ya kawaida binti wa miaka 17 Vumilia Kyando mkazi wa Makete mkoani Njombe amemnyonga na kumtumbukiza kwenye mto mwanaye wa kumzaa John Kyando kwa sababu ya kupata mchumba .

Mto

Binti huyo ambaye alikuwa anajishughulisha na kazi ya kuuza ‘bar’ alimpata mchumba ambaye alikuwa siyo baba wa mtoto huyo ambapo alikuwa tayari kuishi naye lakini hakumtaka mtoto huyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi Podinsiana Protas amesema kuwa binti huyo alifikia maamuzi ya kumuua mwanaye wa kumzaa baada ya mwanaume ambaye alitaka kumuoa kumtaka awe naye peke yake.

Aidha Kamanda amefafanua kuwa mwanamke huyo anahojiwa na Jeshi la polisi na upelelezi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili