Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Amuua Mkewe kwa madai ya kutumia (ARV) kwa kificho

Jumamosi , 8th Mei , 2021

Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Peter Elias (29) mlinzi na mkazi wa Ndembezi Mjini Shinyanga kwa kosa la kumuua mke wake Pili Luhende akimtuhumu kutumia Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) kwa kificho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea Mei 3,2021 majira ya saa nne na nusu usiku katika mtaa wa Dome, Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga tulipokea taarifa kuwa Pili Luhende, aliuawa na Peter Elias (29), mlinzi na mkazi wa Ndembezi ambaye ni mume wake baada ya kumpiga. Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kuhojiwa ambapo tarehe 06/05/2021 alionyesha alipoutelekeza mwili wa marehemu maeneo ya Mwagala darajani,” ameeleza Kamanda Magiligimba.

"Pia alibainisha kuwa alimpiga kwa kutumia ngumi na chanzo kikiwa ni mtuhumiwa kumbaini mkewe anatumia dawa za HIV yaani ARV kwa kificho hivyo ikamtia hasira na wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara kuhusiana na hilo,” ameongeza .

Amesema mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umeharibika na umekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava