Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Justus Kamugisha.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Justus Kamugisha, amesema kijana huyo ametekeleza mauaji hayo akidai kuwa wazazi wake hao ni wachawi.
Kamanda Kamugisha amesema kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo jeshi la polisi lilifanya mahojiano na kijana huyo na amekiri kutekeleza mauaji hayo na lengo lake lilikuwa ni kuwauawa wote wawili kwa kuwa wanashirikiana kumroga.
Kamanda Kamugushi ameeleza kuwa hali ya mama huyo ambae amejeruhiwa na kijana huo ni mbaya na yupo katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya uangalizi na matibabu zaidi.
Kwa upande wake mchambuzi wa masuala ya Kijamii mkoani Mbeya, Bw. Phelemon Mwansasu, amesema kuwa ni vyema madhehebu ya dini yakaongeza juhudi ya mafundisho hususani kwa vijana ili wawe na imani ya kumuogopa Mungu zaidi.