Jumatano , 7th Aug , 2024

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni mkoani humo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne Muliro

watano kuwa amekutwa tayari kashafariki dunia.

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Agosti 7, 2024 na kusema binti huyo anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na kwamba uchunguzi wa tukio bado uanendelea.

Aidha Kamanda Muliro amesema wanaendelea na uchunguzi kwa waliohusika kwenye tukio la ubakaji na ulawiti.