Alhamisi , 23rd Feb , 2023

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema kwamba mtembea kwa miguu aliyegongwa na basi la mwendokasi siku ya jana Februari 22, 2023, katika eneo la Kisutu Dar es Salaam, amelazwa ICU.

Mtembea kwa miguu aliyegongwa na mwendokasi

Taarifa hiyo imeeleza kwamba mwanaume huyo amevunjika mguu, mkono na kuumia kichwani lakini anafungua macho.

Mwanaume huyo amepewa jina la 'Unknown' kwa sababu mpaka sasa hakuna taarifa zake rasmi.