Jumatano , 17th Nov , 2021

Emanuel Isack ambaye ni mchimbaji katika mgodi wa Mhalo uliopo wilayani Kwimba mkoani Mwanza, amefukiwa kwenye duara alilokuwa anachimba dhahabu siku tisa zilizopita na jitihada za kumtafuta mchimbaji huyo bado zinaendelea.

Duara

Musa Sitta ni mchimbaji katika mgodi wa Mhalo ameeleza namna tukio la Emanuel kufukiwa kwenye duara lilivyotokea kwa kusema kwamba nguzo ya kuingilia chini ya duara ilikatika baada ya mawe kuporomoka hali iliyopelekea vifusi kushuka chini.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 8, 2021, majira saa 9:30 usiku.