Alhamisi , 21st Jul , 2016

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Kanga, kata ya Ipinda katika Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kurukiwa na samaki aina ya Perege mdomoni wakati akiwa anavua samaki ndani ya Ziwa Nyasa.

Ramani ya wilaya ya Kyela

Marehemu aliyefahamika kwa jina la Robert Mwaijenga mwenye umri wa miaka 47, alirukiwa na samaki huyo ambaye baadaye alikwama shingoni mwake na kumsababishia kifo.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Mganga mkuu wa Kituo cha Afya cha Ipinda Dokta, FRANK MWAKALUNDWA, amekiri kumkuta samaki shingoni mwa marehemu baada ya kumfanyia upasuaji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho SAMWEL MWAKAJUNGWA, amekiri kutokea kwa tukio hilo huku shuhuda wa tukio hilo EMMANUEL MWAMGUNDA, akieleza kuwa lilimpata wakati akiwa kwenye shughuli za uvuvi kwenye Ziwa Nyasa.

Wasikilize hapa;-

Sauti ya Dkt FRANK MWAKALUNDWA
Sauti ya Shuhuda wa tukio hilo EMMANUEL MWAMGUNDA