Aliyefariki kwa kukanyagwa na Tembo
Marehemu alikuwa ni dereva wa boda na kwamba alikodishwa kupeleka abiria kijiji cha jirani Orkiushibour Kata ya Ndedo Tarafa ya Makame.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara RPC George Katabazi ameeleza kuwa, watu hao ni jamii ya kifugaji Maasai ambao huishi kwenye hifadhi ya WMA ambayo ina wanyama wengi kama vile tembo na nyati.
Kamanda Katabazi amewataka wananchi hao kuchukua tahadhari kwa wanyama hao wakali akiwaasa kutotembea nyakati za usiku kama walivyokuwa hao.