
Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo nchini Tanzania kimesema kuwa kinakusudia kufanya mikutano ya hadhara katika miji mikubwa nchini kwa kushirikiana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi -UKAWA, kuongea na wananchi juu ya wabunge waliotolewa nje ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tamko hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT- Wazalendo Sabini Richard wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya hatua iliyochukuliwa na chama hicho kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa bunge Kidemokrasia.
Mikutano hiyo imetajwa kuanzia jijini Dar es salaam na baadae kuelekea sehemu mbalimbali katika miji mingine mikubwa nchini Tanzania.