Jumatatu , 25th Jan , 2016

Umoja wa Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo wa Jijini Dar es Salaam umesema umeshtushwa na kiasi kidogo cha fedha kinachotengwa na serikali kwa ajili ya kutekelza mpango wa elimu bure.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe

Katika taarifa yao waliyoitoa kwa vyombo vya habari jana Jijini Dar es salaam umoja huo umesema kuwa kiasi hicho cha fedha kilichotengwa ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji muhimu ya upatikanaji wa elimu bora nchini.

Ngome hiyo ya Vijana wa ACT Wameitaka serikali iongeze kiasi cha ruzuku ili kukidhi dhana ya elimu bure na mahitaji ya shule hadi kufikia sh.elfu 40 kwa kila mwanafunzi wa sekondari na sh. elfu 25 kwa mwaka kwa mwanafunzi wa shule ya msingi.

Aidha katika taarifa yao hiyo vijana hao wameziomba kamati za shule za wazazi kufuatilia kwa karibu fedha hizo za ruzuku na matumizi yake kwa shule husika ili kuepuka ubadhilifu wa aina yoyote.