Jumanne , 27th Sep , 2022

Kijana Sadick Mwashambwa (24), mkazi wa Kitongoji cha Kamficheni, Kata ya Hasamba wilayani Mbozi mkoani Songwe, ameuawa kwa kuchinjwa shingoni baada ya kuvamiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia Septemba 25, 2022, akiwa amelala huku  mke wake akishuhudi tukio hilo.

Jeneza liliboba mwili wa Sadick Mwashambwa

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi mkoani Songwe, limesema kwamba tayari linawashikilia watu wanne huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Siku ya tukio imeelezwa kuwa baada ya watu wawili kufika nyumbani kwa marehemu na kisha kummchinja, watu hao waliondoka bila kuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Alex Mkama, amesema marehemu aliuawa kwa kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali.