Ijumaa , 10th Apr , 2015

Abiria  zaidi 1000 mjini Musoma wameshindwa kusafari baada ya  madareva kuitisha mgomo.

Abiria  zaidi 1000 walikuwa wakisafari kutoka Musoma kwenda Dar es salaam kupitia mikoa ya Mwanza na Shinyanga  na wale  wa kwenda mpakani mwa Tanzania na Kenya Sirari pamoja na wa  ndani ya mkoa wa Mara wameshindwa kusafari baada ya  madareva kuitisha  mgomo.
 
Baadhi ya madereva  ambao  wamekutwa  katika kituo kikuuu  cha  mabasi ya Bweri mjini Musoma,wamesema kuwa mgomo huo  umeitishwa  kwa ajili  ya  kupinga agizo la serikali la kukataa kusajili upya  leseni  zao hadi baada  ya  kwenda kusoma katika  vyuo  vinavyotambulika serikalini.

Kwa upande  wao baadhi ya abiria wamesikitishwa  na mgomo huo  wa madereva  ambao  umesababisha  hata  wagonjwa kushindwa kusafiri hivyo  wameitaka serikali  kuchukua hatua  za kumaliza  migomo  hiyo ambayo  wamesema  imekuwa  kero  kubwa  kwa wananchi.
 
Abiria  hao wameshuhudiwa wakiwa wamesimama  kwa  makundi  katika kituo  hicho kikuu cha mabasi huku  magari  makubwa  ya abiria  yakishindwa  kuingia  kabisa  kituoni  hapo   hatua  ambayo  imesabisha  baadhi  ya  abiria  wakilazimika kukodisha  magari madogo aina ya taxi kwenda  jijini Mwanza kwa gharama  ya shilingi  laki nne  kutoka laki mbili za kawaida.