Jumatatu , 27th Jun , 2022

Baadhi ya wawekezaji wazawa  nchini wamesema sera ya Serikali katika kudhibiti maradhi ya milipuko iliyowekwa katika uchumi  imesaidia kuimarisha  uwekezaji hivyo kuwataka wazawa kujitokeza zaidi kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo miradi ya kisekta.

Hayo yamejiri wakati kituo kilichopewa hadhi ya kusimamia uwekezaji kikisimamia kauli mbiu  mbalimbali ikiwemo nafasi ya Mapinduzi ya nne ya Viwanda katika masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshaji wakati na baada ya Janga la Corona hali iliyofanya uwekezaji kuzidi kuimarika.

Akitoa taarifa ya hali ilivyo Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wawekezaji Bi. Anna Lyimo akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) amewakaribisha wananchi na wawekezaji kutembelea ofisi hizo ili kupata elimu juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na tafiti mbalimbali zinazoibua fursa za Uwekezaji nchini.

Takribani wageni zaidi ya 50 wameweza kupata elimu juu ya fursa za uwekezaji na namna mbalimbali za huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji hasa kupitia Kituo cha Mahala Pamoja ( One Stop Facilitation Centre).kwa wiki pekee ya utumishi.