
Meneja mradi wa utengenezaji wa mfumo wa single window Robert Mtendamema,
Hayo yamebainishwa mara baada ya majadiliano ya wakuu wa taasisi 12 ambazo zinahusika katika utoaji wa vibali vya uwekezaji hapa nchini kuangalia namna ya kutengeneza mfumo mzuri ili kuwawezesha wawekezaji kupata vibali kwa urahisi zaidi ambapo Meneja mradi wa utengenezaji wa mfumo wa single window Robert Mtendamema, amesema kuanzia Juni 15 mwaka huu mfumo huu utaanza kutumika.
"Tumechelewa kuanza ila sasa mfumo huu wa pamoja unakwenda kuwa kivutio kikubwa kwa wewekezaji kutoka nje na ndani," amesema Mtendamema.
Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Taarifa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mafutah Buniri, amesema mfumo huo utasaidia kurahisisha katika utoaji wa huduma.
"Kituo tayari kimetoa eneo la uwepo wa wataalamu kutoka taasisi hizi 12 ili ziweze kutoa huduma ya pamoja,"amesema Mafutah
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Dkt. Yusuph Ngenya wameeleza namna mfumo huu utakavyoondoa usumbufu kwa wawekezaji kupata vibali.