Ijumaa , 17th Jun , 2022

Mfanyabiashara mmoja mkoani Katavi ameshangaza wengi baada ya kujitokeza mtaani na kutangaza kununua mbegu za Upupu kwa shilingi 12,000  kwa kilio moja, jambo ambalo limefanya wananchi wa mkoa huo kuingia porini kusaka zao hilo linalojulikana kwa machungu yake ya kuwasha.

Inaelezwa kuwa mnunuzi huyo anayenunua kilo moja kwa shilingi 12,000 bei ambayo inatajwa kuwa juu kuliko mazao yote anasafirisha kwenda Zanzibar kwa ajili ya shughuli za kuzalisha malighafi ambazo inaelezwa kuwa ni dawa kwa binadamu.

Baadhi ya mashuda wa mbegu z upupu zikinunuiwa na wauaji kulipwa fedha kubwa ,wameshanga nakuhamasika kuingia porini kwa ajili ya kuvuna zao hilo.