Wafanyabiashara waomba maeneo kwa ajili ya miradi ya viwanda.
Wamesema Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiagiza bidhaa kutoka nje ya nchi lakini kukiwa na viwanda nchini kutasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na kuitangaza Tanzania.
“Tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo na eneo la biashara litakalotukutanisha pamoja na kuweka viwanda ili na mataifa mengine yaweze kuja kufata bidhaa nchini kwetu”, alisema Abdallah Mwinyi.
“Kiwanda kimoja kinazalisha zaidi ya ajira 1000, nchi yetu kila mwaka wanafunzi wanamaliza vyuo na ajira bado ni changamoto kwahiyo tukipata hii nafasi tutaisaidia Serikali kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana”, alisema Riziki Ngaga,Katibu Jumuiya ya Wafanyabiashara.
Tunaomba Serikali iweze kuunga mkono juhudi hizi kwa kutuwekea miundombinu rafiki Kama wakitupatia eneo hilo ili tutakapoanzisha mradi tuweze kutekeleza kwa wakati uliokusudiwa”, alisema Alfred Lyandi, Mtaalam wa Jumuiya ya Wafanyabiashara.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo anasema kwa kushirikiana na wizara Nyingine za kisekta watapunguza changamoto za uwekezaji nchini.
“Wizara ya viwanda tunashirikiana na wizara ya uwekezaji, wizara ya fedha tutasngalia changamoto gani zinakwamisha kwa pamoja tutazitatua ili kuhakikisha tunatoa nafasi kwa wawekezaji wa ndani na wanakuza mitaji yao “, alisema Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara.