
Mradi wa gesi asilia
Wananchi na wakazi wa vijiji hivyo wametakiwa kutoa ushirikiano kwa shirika la maendeleo ya petroli Tanzania ( TPDC) kwa ajili ya kufanya tathimini ya mali, na kulipwa fidia zao, kwa ajili ya kuanza utekelezaji mradi huo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Moma kata ya Moma wakati wa kutambulisha mradi huo, Mkuu wilaya ya hiyo, Dustan Kyobya amewataka wananchi kupokea mradi huo, huku Emmanuel Simon meneja gesi asilia toka shirika la maendeleo ya petroli Tanzania, akieleza namna ambavyo matumizi ya gesi asili yameongezeka kutokana na kuwapo kwa ukame hapa nchini.
Baadhi ya wananchi wakazungumzia uwapo wa mradi huo katika vijiji vyao, wamesema ni mradi muhimu na kwamba serikali na wawekezaji wajitahidi kuhakikisha vijiji vinavyopitiwa na mradi huo vinawanufaisha wakazi wa maeneo hayo kwa kutoa fursa za kujiingizia kipato kwa wenyeji.