Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Tuweke mikakati kupambana na ukosefu wa Chakula"

Jumatatu , 23rd Mei , 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amesema katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani, nchi za bara la afrika zinaweza kufanya uwekezaji mkubwa katika kilimo na kuweza kutosheleza mahitaji ya chakula duniani.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani linalofanyika Davos nchini Uswisi alipochangia mada ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani. Amesema nchi za Afrika kutokana na kujaaliwa ardhi pamoja na maeneo ya uzalishalishaji katika sekta ya kilimo zinapaswa kuboresha sera ili ziwe rafiki katika kilimo ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula.

Aidha Makamu wa Rais ameongeza kwamba nchi za Afrika zinapaswa kuwekeza  katika kilimo cha umwagiliaji na himilifu, kuwekeza katika miundombinu ikiwemo barabara  pamoja na kutenga ardhi kwaajili ya kilimo cha mashamba makubwa pamoja na wawekezaji. Ameongeza kwamba kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi kuna ulazima wa kuwekeza katika viwanda vitakavyozalisha pembejeo ikiwemo mboleo na mbegu.

Makamu wa Rais ameziasa taasisi za kimataifa za utafiti kuungana mkono jitihada za nchi za Afrika katika kuboresha afya ya udongo ili kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo. Aidha amesisitiza umuhimu wa suala la amani duniani ili kutoa fursa ya uzalishaji na usambazaji wa chakula duniani., 

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Tanzania inapanga kutumia rasilimali watu hasa vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo kwa kutenga maeneo ya kilimo yatakayokwenda sambamba na huduma za pamoja kama vile huduma za ugani, pembejeo na masoko. 

Mada hiyo imejadiliwa kutokana na dunia kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea upungufu wa chakula duniani kama vile Uviko19, vita pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais yupo Davos nchini Uswisi kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaoshirikisha wakuu wa nchi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa pamoja pamoja na wafanyabiashara.
 
HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava