Jumanne , 28th Sep , 2021

Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kusambaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Tehama, kuibua na kukuza vipaji vya wabunifu na kuwarahisishia watu upatikanaji wa huduma mbalimbali.

Tume ya Tehama (ICT Commission)

Sasa ili kukuza uelewa zaidi, Tume ya Tehama (ICT Commission) imepanga kuwakutanisha wadau mbalimbali wa ICT ili kuonyesha bidhaa zao, huduma na ubunifu wa Tehama na kuimarisha mahusiano kati ya watalaam wa Tehama Tanzania na wadau wengine nje ya nchi katika mkutano mkuu wa mwaka wa Tehama 2021 (TAIC 2021) utakaofanyika Arusha kuanzia Oktoba 20.