Jumanne , 2nd Aug , 2022

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wakulima kutumia fursa za mitandao katika kujikwamua kiuchumi kwa kutafuta huduma mbalimbali kama huduma za masoko ya mazao wanayozalisha na yale yanayopatikana katika maeneo yao.

Wakulima wakiwa katika shughuli za kilimo

Akizungumza katika banda la TCRA, mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Asajile John amesema matumizi bora ya mitandao yana faida kubwa ikiwa wakulima wataitumia vizuri.

Asajile ameongeza kwamba wanatamani kuona asilimia 80 ya watumiaji wa simu za mkononi wanafikiwa na huduma za mitandao na kwamba Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu ni muhimu kwa wakulima pia kwasababu itarahisisha huduma bora za mawasiliano katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya mashambani.