Alhamisi , 14th Nov , 2024

Katika kuhakikisha Rasilimali za nchi zinaongezwa thamani na kuitangaza Tanzania, Serikali imekuja na mkakati wa kuongeza thamani ya Madini ili kuchochea uanzishwaji viwanda vitakavyokuwa na manufaa nchini.

Antony Mavunde, Waziri wa Madini

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini , Antony Mavunde wakati anaongea na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya Madini unaotarajiwa kufanyika Novemba 19-21, 2024.
“inalenga kuhimiza umuhimu wa uongezaji thamani wa madini kama njia ya kuleta faida zaidi za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo endelevu ya taifa letu na dunia, kupandisha thamani ya madini yanayozalishwa nchini kabla ya kusafirishwa nje kwa lengo la kuchochea uanzishwaji viwanda vitakavyokuwa na manufaa nchini, kwa majirani wanaotuzunguka na duniani”, Antony Mavunde, Waziri wa Madini.

Aidha Mavunde anasema, Mkutano utaangazia  fursa zilizopo kwenye Madini mengine ya Viwandani na ujenzi.
“Onesho hilo pia litaangalia namna madini yanavyojifungamanisha na sekta nyingine kutoka viwandani hadi kwenye matumizi ya kawaida, na jinsi yanavyoweza kuchochea maendeleo kwa watanzania na ulimwengu kwa ujumla”, Antony Mavunde, Waziri wa Madini.

Kuhusu rasilimali za nchi kutumika kikamilifu, baadhi ya wananchi wanatoa maoni mseto kuhusu sekta ya Madini nchini.
“Nashauri Madini ghafi yasiuzwe nje ya nchi badala yake yaongezewe thamani hapahapa ili biashara ifanyike hapahapa nchini ili kupata wageni na kuongeza mzunguko wa fedha”, Godwin Myovela, Mkazi wa Dar es Salaam

“Watanzania wapewe kipaumbele katika sekta ya Madini, kwa sababu Madini yanahitaj fedha kwahiyo wawezeshwe mitaji ili waweze kutengeneza uchumi utakaosaidia nchi yetu", Godson Kiliza, Mkazi wa Dar eś Salaam