Ijumaa , 30th Sep , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imewataka wadau wa taasisi za fedha nchini kuongeza upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuhakikisha kuwa wanapata mikopo yenye tija itakayowasaidia kuongeza mitaji yao na kukuza uchumi.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo nafuu kutoka benki ya UBA ijulikanayo kama Mkopo Kitonga na kubainisha kuwa sekta ya wajasiriamali wadogo na wakati nchini ina mchango mkubwa wa kutatua changamoto ya ajira nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya UBA, amesema bidhaa hiyo mpya ya mikopo waliyoizindua leo imejali wateja wake na wajasriamali ambapo itasaidia kupata mikopo nafuu na kukuza mitaji ya biashara zao.