Jumatatu , 14th Feb , 2022

Mkuu wa kitengo cha masoko kutoka DStv Baraka Shelukindo, amesema kwamba takribani nchi 32 zitakuwa zinaiangalia chaneli ya East Africa TV kupitia chaneli namba 384, baada ya kuanza kuonekana rasmi hii leo.

Mkuu wa kitengo cha masoko kutoka DStv Baraka Shelukindo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 14, 2022, mara baada ya kufanya uzinduzi huo ikiwa ni mara ya kwanza kwa East Africa TV kuonekana katika king'amuzi cha DStv.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko kutoka East Africa TV Roy Justo, amemshukuru Rais Samia kupitia kwa Waziri wa Habari Nape Nnauye, kwa kuruhusu na kuwezesha watanzania waliowengi kupata chaneli za bure kupitia king'amuzi hicho.