Mkaguzi wa mahesabu ya serikali, Sandra Chogo
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 19, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, wakati akitoa elimu ya masuala ya bitcoin na Crypto currency, na kusisitiza Watanzania wasikimbilie tu kuweka pesa bali wafanye uchunguzi kwanza.
"Thamani ya bitcoin asubuhi ya leo nimeangalia kwa Tshs ilikuwa inasoma bitcoin moja ni milioni 98," amesema Sandra.
Aidha ameongeza kuwa, "Bitcoin ina kama miaka 13 na kibaya zaidi mwanzilishi wake hatumjui na napenda kuwaambia Watanzania kwa kutomjua mwanzilishi kila mtu kwa nafasi yake asome kwa undani hichi kitu ili tujue nyuma yake kuna nini na sio kukimbilia kuweka pesa, system ikifungwa utamlilia nani,".