
Tuzo ya dhahabu ya TBL
ilishinda mapema wiki iliyopita.
Hii inafuatia tetesi zilizosambaa hapo jana kuwa Tuzo hiyo haijulikani ilipo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jumapili, Meneja wa Brand za TBL, Pamela Kikuli alisema kuwa, TBL baada ya kuwapa fursa Watanzania kuiona Tuzo hiyo katika maeneo ya Mbagala Rangi Tatu, Kituo cha Mabasi cha Morocco, Karume na Buguruni watatoa tamko rasmi kuhusiana na maoni ambayo wameyapokea katika maeneo hayo kutoka kwa Watanzania.
Aliongeza kwa kusema kuwa Waandishi wa Habari wote wanakaribishwa kesho katika kituo cha mabasi Morocco, kuanzia mida ya saa nane na nusu mchana.
Bidhaa zinazozalishwa na TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redds Original, Budweiser, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Grand Malt na Safari Sparkling Water.
TBL group imeorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam, ikiwa na wafanyakazi takriban 1,700, inafanya uzalishaji katika mikoa minne ikiwa na vituo kadhaa vya usambazaji wa bidhaa zake.
Ujumbe wa Piere Likwidi na @LilOmmy , baada ya kujionea tuzo ya dhahabu iliyoshinda kampuni ya Utengenezaji wa bia TBL.
Kesho Februari 28, 2020 tuzo hiyo inatarajiwa kuwepo maeneo ya Karume Ilala - Dar es salaam, kwa ajili ya watanzania kujionea tuzo yao. #KiziboChaTBL pic.twitter.com/uuxdp9epvo
— East Africa TV (@eastafricatv) February 27, 2020