Hali ya uwepo wa ukame kwa baadhi ya maeneo nchini wafanyabiashara wa nafaka wanaueleza kama somo ambalo seerikali inapashwa kulichukua ili kuchagiza kwa kasi kilimo cha umwagiliaji ambacho kitakuwa suluhu kwa watanzania wakibainisha kuwa Tanzania iko na mabonde mengi kila ukanda hivyo leo isingehangaika na uhaba wa mazao.
Hata ivyo wauzaji wa mchele na maharage sokoni hapo wamesema usafirishaji bado uko juu hadi 13000 kutoka 12000 kwa gunia ikisafirishwa kutoka mbeya wakibain isha hali ni ngumu kwa wananchi wa kima cha chini.
Hivi karibuni wizara ya kilimo kupitia kwa naibu waziri wake Antony Mvunde ilisema kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kuanza miradi ya umwagiliaji ili kuwaondoa wakulima katika hatari ya mabadiliko ya tabia nchi.