Jumatatu , 29th Mei , 2023

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania  imewataka wateja wake kuendelea kutumia mtandao huo kwa kufanya miamala ya kifedha ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zitakazobadilisha maisha yao kibiashara na kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na meneja  uhusiano na mawasiliano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando wakati akitangaza washindi wa  promosheni ya upige mwingi na Airtel inayotarajia kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo  wateja wanajishindia zawadi mbalimbali ikiwepo pesa taslimu,friji,pikipiki na flat screen..

Mbando amesema kuwa mpaka sasa kampeni hiyo imeshatoa washindi  wa fedha taslimu milioni 15 na zawadi zingine zinaendelea kutolewa ambapo mpaka sasa imebakia miezi miwili na siku 15 ,kati ya miezi mitatu ambayo kampeni itaendeshwa  ambapo  kila mteja au wakala wa airtel anaponunua bando au kufanya muamala wowote kutumia airtel money ataingia kwenye droo ya kushinda zawadi.