Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete akionesha kitabu cha sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, katika tukio la uzinduzi wa sera hiyo jijini Dar es salaam, mwezi Feb. mwaka 2015.
Mkuu wa Mahusiano Umma na Vyombo vya Habari wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Annette Kanora (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Benki ya NBC yanayolenga kufanikisha maandalizi ya msimu wa tano wa mbio za NBC Dodoma Marathon. Mbio hizo zenye hadhi ya kimataifa zinatarajiwa kufanyika Julai 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkuu wa Mahusiano ya Umma ya Umma na Mawasiliano wa NBC, Godwin Semunyu