James Mbatia
Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na Rais Jakaya Kikwete, chama cha NCCR Mageuzi kimesema sera hiyo haina manufaa yenye tija kwa wananchi bali sera hiyo imelenga uchaguzi mkuu kwa kuwalaghai wapiga kura na sio kutekeleza yaliyomo ndani ya sera hiyo.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi taifa Mh James Francis Mbatia ameyabainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam wakati akieleza masuala mbalimbali yaliyoanishwa ndani ya sera mpya ya elimu ambayo imeandaliwa kwa muda wa miaka saba hadi kukamilika kwake na kuzinduliwa Februari 13 mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete na kuanisha mpango wa serikali wa kutoa elimu bure pindi sera hiyo itakapoanza kutumika jambo ambalo amelieza kuwa ni kutendawili kisichokuwa na jibu kamwe.
Kuhusu muda wa kipindi cha miaka saba kilichotumika kuiandaa sera hiyo hadi kukamilika kwake Mh Mbatia amesema ni muda mrefu umetumika huku sera ikiwa imegubikwa na makosa mengi ya uchapaji pamoja na kushindwa kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya sasa duniani hivyo sera imeshapitwa na wakati hata kabla haijaanza utekelezaji wake kwa wananchi.