Yanga yazidi kujipa Matumaini ya Ubingwa
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga wamesema bado hawajakata tamaa ya kutetea ubingwa wa ligi hiyo ambayo sasa inaongozwa na Azam Fc inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza msimu huu.