Mchakato wa mabadiliko ya katiba Simba SC.
Klabu ya Simba ya jijini DSM, iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya katiba yake kufuatia mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika mapema mwezi uliopita katika viwanja vya bwalo la maafisaa wa polisi la Oysterbay.
Akiongea na muhtasari wa michezo, katibu mkuu wa klabu hiyo, bwana Ezekiel kamwaga amesema kimsingi mchakato huo umeshatoka klabuni na uko kwenye ngazi za juu zaidi.