Mashali asaini kuzichapa na Nyilawila.
Mabondia Thomas Mashali na Kalama Nyilawila, wamesaini mkataba wa kupanda ulingoni kuwania ubingwa wa UBO-Continental, katika pambano la raundi 10 litakalofanyika Mei 1,2014, katika ukumbi wa Karume ndani ya viwanja vya maonesho ya Mwalimu Nyerere.