Monday , 26th May , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ras Six ambaye anaiongoza bendi maarufu ya walemavu inayoitwa 'Tunaweza Band' anatarajia kuungana na bendi yake kuanzisha mradi uitwao 'Sanaa dhidi ya umaskini'.

Ras Six ambaye ni mlemavu wa ngozi ameielezea eNewz kuwa mradi huu mpya utakuwa pia ukipewa sapoti na mashirika mbalimbali yaliyojitolea kuwasaidia walemavu hao yaitwayo CEFA na Vipaji Foundation.

Ras Six hivi sasa amefyatua single yake mpya inayoitwa 'NO' ambayo imerekodiwa na mtayarishaji maarufu nchini Fundi Samweli na ipo mbioni kutoka rasmi mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.