Jumatatu , 6th Oct , 2025

Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi inafuatia taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu wa Humphrey Polepole zikidai kuwa ametekwa na kwamba tayari limeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo ili kupata ukweli.

Kufuatia Habari za kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humprey Polepole, Jeshi la Polisi limesema linafuatilia taarifa za madai hayo.

Jeshi la Polisi katika taarifa yake iliyotolewa leo Jumatatu, Oktoba 6, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi linachunguza taarifa zinazosambaa mitandaoni kutoka kwa baadhi ya ndugu wa Polepole wanaodai ametekwa huku likisema kuwa, hatua za uchunguzi wa awali zinaendelea ili kubaini ukweli wa madai hayo. 

Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi inafuatia taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu wa Humphrey Polepole zikidai kuwa ametekwa na kwamba tayari limeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo ili kupata ukweli.

Awali, Bwana Humprey Polepole alitumiwa wito wa kisheria kutakiwa kuripoti ofisini kwa DCI ili kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao ya kijamii , agizo ambalo hakulitekeleza mpaka sasa.