Polisi wakamata silaha iliyotumika kwa mauaji
Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kukamata silaha mbili ikiwemo aina ya SMG iliyotumika katika tukio la ujambazi ambalo lilisababisha kifo cha askari polisi na mwengine kujeruhiwa vibaya mwezi uliopita kwenye ukanda wa Kitalii eneo la Pongwe.