Mkapa Aonya Udini na Ukabila Afrika Mashariki
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa amewataka wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokubali kuruhusu chokochoko za kikabila, kisiasa na kidini zinazoweza kuleta machafuko na kupelekea mauaji ya kimbari.