Rais Kikwete ajivunia Muungano wa Tanzania.
Tanzania leo inasherehekea miaka 50 ya Muungano wa kihistoria wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika uwanja wa taifa kwa gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama na kukaguliwa na amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Kikwete.