Tanzania yapinga kuondolewa kwa spika EALA
Wabunge saba wanaoiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki wamesema wanapinga mpango wa kuondolewa kwa spika wa bunge hilo Margaret Zziwa kutokana na hoja zilizotolewa dhidi yake kuwa kinyume na malengo ya Jumuiya hiyo.

