Tuesday , 10th Jun , 2014

Wabunge saba wanaoiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki wamesema wanapinga mpango wa kuondolewa kwa spika wa bunge hilo Margaret Zziwa kutokana na hoja zilizotolewa dhidi yake kuwa kinyume na malengo ya Jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki alhaji Adam Kimbisa (kulia) amesisitiza mpango wa Tanzania kutounga mkono azimio la kumuondoa spika Zziwa.

Akizungumza Jijini Dar-es-Saalam Mwenyekiti wa wabunge hao Mhe. Adam Kimbisa, amesema hoja zilizotolewa kwa ajili ya kumuondoa Spika huyo hazijafata sheria na hazina maslahi kwa wananchi wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Tanzania Mh. Shyrose Bhanji ambae hapo awali alikuwa ni mmoja kati ya waliotaka kumtoa spika huyo amesema amebadili maamuzi baada ya kugundua kuwa kuna ajenda ya siri katika suala hilo.