Watano wanashikiliwa kwa uvamizi kituo cha polisi
Polisi mkoa wa Pwani nchini Tanzania, inawashikilia watu watano, kwa tuhuma za kuhusika katika tukio ambapo watu wasiofahamika walivamia kituo kidogo cha polisi cha Mkamba Wilayani Mkuranga na kumuua askari polisi mmoja, kujeruhi na kuiba bunduki 5.

